Klabu ya Man Utd, imetangaza namba za jezi za wachezaji watakazo zitumia katika michezo ya ligi kuu ya soka nchini England pamoja na michuano ya Europa League msimu wa 2016/17.

Mshambuliaji kutoka nchini Sweden, Zlatan Ibrahimovic, aliesajiliwa klabuni hapo kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na klabu ya bingwa nchini Ufaransa PSG, atavaa jezi namba 9, na Anthony Martial aliyekua anatumia namba hiyo msimu uliopita amebadilishiwa na kukabidhiwa namba 11.

Hata hivyo katika mlolongo wa jezi hizo, hakuna namba sita, na tayari imeanza kuhisiwa huenda namba hiyo imeachwa kwa makusudi ili ije kutumiwa na kiungo kutoka nchini Ufaransa na klabu bingwa nchini Italia Juventus, Paul Pogba.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23, anahusishwa na mipango ya kurejeshwa Old Trafford kwa ada ya Pauni milioni milion 100, ambayo itavunja rekodi ya dunia.

Roberto Mancini Aguswa Na Mkasa Wa Mario Balotelli
Kikwete apongeza ‘Kili Challenge’ ya GGM, ataka Tanzania iwe ya kwanza kutokuwa na maambukizi ya VVU