Gwiji wa Manchester United, Paul Scholes anaamini kuwa Anthony Martial hana moyo wa kuichezea klabu hiyo na hafai kuwa kikosi hapo kwa siku za usoni.

Hii ni kutokana na Martial kushindwa kuibeba Man United hasa katika eneo la ushambuliaji la kikosi hicho.

Martial alirejea uwanjani hivi karibuni lakini amekuwa hana mchango ndani ya kikosi hicho chini Erik ten Hag.

Scholes amesema Martial amekuwa hana ule moyo wa kujitoa kwa ajili ya klabu yake hiyo.

“Nafikiri nafasi straika kwa sasa ipo wazi kwa jinsi mambo yalivyo kwenye timu.”

“Anthony Martial ana kipaji hilo liko wazi nafikiri pale panapokuwa na ugumu anaonekana kuwa hana ule moyo kujitolea hana na hafanyi hivyo kwa ajili ya Man United.”

“Japo Man United ina matatizo maeneo tofauti kama beki wa kulia ambapo pia sio kama Wan-Bissaka (Aaron) na Dalot (Diogo) kama wote wanastahili kuwa pale.”

“Kuhusu kipa hakuna asiyemfahamu David de Gea kama ni kipa mzuri japo ubora wake kwa sasa kama umeshuka hivyo United inatakiwa ikifikirie kama maendeleo yao.”

Yahya Mbegu: Nina mtihani mkubwa usajili Bongo
Arteta apaza sauti safari ya Etihad Stadium