Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Burkina Faso Paulo Duarte amethibitisha kufanya mazungumzo kwa njia ya simu na meneja wa Man Utd Jose Mourinho, kabla ya mchezo wa nusu fainali dhidi ya Misri uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo mjini Libreville nchini Gabon.

Duarte aliwaambia waandishi wa habari, alizungumza na Jose Mourinho na jambo kubwa alilomuomba ni kumfikishia ujumbe kwa wachezaji wa Burkina Faso.

Alisema Mourinho aliwatia moyo wachezaji wa Burkina Faso, na yeye kama mkuu wa benchi la ufundi aliyatumia maneno ya meneja huyo kutoka nchini Ureno katika mawaidha yake ya mwisho kabla ya kuingia uwanjani kupambana na Misri.

Hata hivyo amesema kitendo cha Jose Mourinho kumpigia simu kilimshtua kutokana na kuamini kwamba, meneja huyo alikua katika majukumu mengine ya kukiandaa kikosi cha Man Utd ambacho usiku wa kuamkia hii leo kilikabiliwa na mchezo wa ligi ya England dhidi ya Hull City.

Duarte alisema alifarijika kuona Mourinho amekua shabiki wa kikosi cha Burkina Faso, na alimthibitishia amekua akifuatilia michezo ya timu hiyo tangu mwanzo wa fainali za Afrika za mwaka huu.

RC apishana kauli na Waziri Loliondo
Wapinzani Kenya waweka mikakati mipya