Imefahamika kuwa Aston Villa inahitaji walau Pauni 60 milioni katika dirisha lijalo la majira ya baridi ili kumuuza kiungo wao Mbrazili Douglas Luiz, ambapo timu nyingi zimeonyesha nia ya kumsajili ikiwamo Arsenal.

Vilevile klabu hiyo ya Villa Park imepanga kufanya naye mazungumzo ili kumsainisha mkataba mpya ambao utawekwa kipengele cha Pauni 110 milioni kwa timu zitakazohitaji kumnunua staa huyu ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2026.

Arsenal ndio inadaiwa kuhitaji zaidi huduma ya fundi huyu ili akazibe pengo la Thomas Partey anayedaiwa kuwa ataondoka katika Januari au mwisho wa msimu.

Inaelezwa kuwa kocha Mikel Arteta ni shabiki mkubwa wa Luiz na ndio amempendekeza akawe mbadala wa Partey.

Luiz ambaye pia anahusishwa na Liverpool, msimu uliopita alicheza mechi 22 za michuano yote na kufunga mabao sita na kutoa asisti nne.

TANAPA yaguswa tukio la mafuriko Hanang'
Simba SC yatahadharishwa Morocco