Uongozi wa FC Barcelona unahitaji Pauni Milioni 70 milioni ili kumuachia mshambuliaji wao wa kimataifa wa Brazil, Raphinha wakati wa usajili wa Majira ya Kiangazi.

Klabu za Newcastle United na Chelsea zote zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili Raphinha ambaye ni miongoni mwa mastaa walioonyesha kiwango bora msimu huu, huku mkataba mkataba wake wa sasana Barca unamalizika mwaka 2027.

Barca inataka kutumia pesa hizo kuboresha zaidi kikosi kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kwa msimu ujao 2023/24.

Barca ambayo imekuwa na msimu mzuri kwenye la Liga mbali ya Raphinha imepanga kuuza pia baadhi ya mastaa wengine kwa ajili ya kupata pesa.

Moja ya usajili unaodaiwa kuwaumiza vichwa mabosi wa timu hii ni ule wa Lionel Messi ambaye wanatamani sana kumrudisha, lakini lazima watatakiwa kuuza kwanza kwani sheria za La Liga zinawabana.

Tangu kuanza kwa msimu huu Raphinha amecheza michezo 45 ya michuano yote na kufunga mabao 10.

Mpole ambariki Mayele, amkataa Baleke
Jurgen Klopp kuboresha safu ya kiungo