Aliyekuwa Nahodha na Beki Simba SC, Boniface Pawasa amewapa ukweli Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo ya Msimbazi wanaobeza kiwango cha Kiungo Mshambuliaji Kibu Denis, akisema Mchezaji huyo bado ana nafasi kubwa ya kuendelea kucheza katika kikosi cha kwanza.

Pawasa amesema kwa jinsi Kibu alivyo na nidhamnu ya kutekeleza majukumu yake uwanjani kama ambavyo anaagizwa na makocha wake ataendelea kuwa chaguo la makocha kokote atakokwenda.

Pawasa ambaye kitaaluma ni kocha amesema Kibu amekuwa ni mchezaji anayekubali mabadiliko ya kocha anayompa na kuyatekeleza kwa kiwango kikubwa.

“Watu huwa nawaona hawafurahii kuona Kibu anacheza lakini kuna kitu hawafahamu hakuna kocha ambaye anaweza kumpuuza Kibu hata kama kuna maeneo anafanya makosa,”amesema Pawasa

“Kibu atacheza sana watu hilo wanatakiwa kutambua, nidhamu ya Kibu ndio silaha kubwa ambayo inamtofautisha na wenzake, ni mchezaji ambaye anachukua kwa kiwango kikubwa maelekezo ya kile ambacho kocha anataka akifanye.

“Anapocheza winga na hata waangalie alivyochezeshwa kama mshambuliaji wa kati akitakiwa kuwa na muda mrefu kucheza eneo la hatari bado alifanya hivyo kwa kiwango kikubwa na akafunga bao ambalo kama amefunga mshambuliaji halisi.”

Hata hivyo Pawasa amemshauri Kocha wa Simba SC Roberto Oliveira ‘Robertinho’ kumrudisha Kibu kucheza kama winga kisha kuanza na Mshambuliaji halisi nmoja.

RC Kindamba ahimiza matumizi ya Fedha kidijitali
Wadakwa wakisafirisha Mifugo Nje kimagendo