Mfungaji wa bao la ushindi katika mchezo wa Uefa Super Cup, Perdo Rodriguez ameonyesha kumpuuza meneja wa FC Barcelona Luis Enrique, ambaye jana jioni alisisitiza kuwa tayari kufanya kazi na mshambuliaji huyo.

Pedro ameonyesha hali hiyo baada ya kuwaambia wachezaji wenzake wa FC Barcelona, yu tayari kuondoka klabuni hapo baada ya kukamilisha kazi ya kuipa ubingwa wa Uefa Super Cup usiku wa kuamkia hii leo, klabu hiyo iliyomkuza tangu akiwa na umri mdogo.

Pedro alifanya hivyo kwa kutambua kazi yake ya kuitumikia klabu hiyo ya Camp Nou, ilikua imefikia tamati hususan mpango wake wa kuelekea nchini England kukwamishwa mara kadhaa katika kipindi hiki, kwa kigezo cha kuhitajika katika mpambano dhidi ya Sevilla FC.

Hata hivyo mshambuliaji huyo anayehitajika Old Trafford kwa kiasi cha paund million 22, hakunukuliwa akizungumza na wenzake maneno hayo, bali wachezaji wa Barcelona walioambiwa na Pedro walivujisha siri hiyo kwa baadhi ya waandishi wa habari, waliokua wakifuatilia shamra shamra za ubingwa huko mjini Tbilisi nchini Georgia.

Enrique, aliwaeleza waandishi wa habari kabla ya mtanange wa Uefa Super Cup, mpango wake wa kutaka kuendelea kufanya kazi na Pedro na aliahidi kukaa nae chini na kukuabliana baadhi ya mambo ambayo yatampa uhuru kwenye kikosi cha Barcelona.

Pedro amekuwa na wakati mgumu wa kucheza kila mara tangu Luis Enrique alipokabidhiwa majukumu ya kuwa mkuu wa benchi la ufundi mwanzoni mwa msimu uliopita, hali ambayo ilikua tofauti na misimu kadhaa iliyopita.

Mfumo wa meneja huyo ulidhihirisha wazi Pedro haitajiki kwenye kikosi chake, kutokana na kuwatumia mara kwa mara washambuliaji watatu Luis Suarez, Neymar pamoja na Lionel Messi.

Lowassa Atahadharishwa Kuhusu ‘Mafuriko Yake’
Stoke City Wakamilisha Usajili Wa Shaqiri