Gwiji wa soka duniani Edson Arantes do Nascimento maarufu kama Pele amesema kuwa mchezaji wa Brazil Neymar alifanya maamuzi sahihi kuondoka Barcelona na kujiunga na klabu ya Paris Saint-Germain.

Neymar alijiunga na miamba hao wa Ufaransa kwa uhamisho ulioigharimu PSG kiasi cha pauni milioni 198 nakuvunja utatu wa ‘MSN’ uliundwa na Messi,Suarez na yeye mwenyewe Neymar.

Pele ambaye alishinda kombe la dunia mara tatu akiwa na timu ya taifa ya Brazil amesema kuwa ni wakati mzuri kwa Neymar kuonyesha kipaji chake akiwa Paris Saint-Germain.

”Kwa sasa mchezaji bora nchini Brazil ni Neymar nafikiri amefanya jambo zuri kuhama Barcelona kwasababu kulikuwa na ushindani mkuwa baina yake na Lionel Messi” alisema Pele.

Pele alishinda kombe la dunia mara tatu akiwa na timu ya taifa ya Brazil

Pele anaamini kuwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anaweza kushinda tuzo ya Ballon d’Or akiwa PSG nakufuata nyayo za Rivaldo, Ronaldo, Ronaldinho na Kaka amabao ni wachezaji wakibrazili walioshinda tuzo hiyo.

Tayari Neymar ameanza kufanya vizuri akiwa na PSG

Akijibu swali baada ya kuulizwa kuhusu Coutinho Pele amesema kuwa mchezaji huyo anacheza vizuri lakini kwa wakati huu Neymar ndiye bora zaidi.

 

 

Spika Ndugai aongoza kikao kamati ya uongozi Dodoma
Acacia kupunguza wafanyakazi migodini