Meneja wa klabu ya Man City , Manuel Pellegrini ameanza kuweweseka na kudai kwamba hatishwi na maamuzi yoyote ambayo yatachukuliwa na viongozi wa klabu hiyo.

Pellegrini aliyasema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari kuwa amekuwa anajisikia vibaya sana kupokea taarifa ya kuondolewa.

Alisema yeye amepewa ajira na viongozi wa klabu hiyo, lakini anafahamu iko siku ataondoka kwenye kazi hiyo na kufanya mambo mengine.

“Ukweli nimechoshwa na nipo tayari kwa lolote, nimekuwa nasikia kuna mipango ya kutaka kuondolewa hapa Man City, sawa hiyo ni kazi ya watu,” aisema kocha huyo.

Kauli hiyo imekuja baada ya kuwepo tetesi kwamba kocha huyo huenda akaondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa sasa wa Beyern Munich, Pep Guardola.

Dylan Kerr: Mnyama Simba Yu Tayari Kuwinda
De Bruyne Afichua Siri Ya Kuachana Na Chelsea