Meneja wa klabu ya Man City, Manuel Pellegrini almanusura angekosa safari ya kuelekea nchini Ujerumani ambapo hii leo kikosi chake kitakabiliwa na mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Borussia Monchengladbach.

Pellegrini alifika kwenye uwanja wa ndege mjini Manchester na kubaini hakua na hati ya kusafiria katika mkoba wake na ndipo alipolazimika kurejea klabuni kusaka mahala alipokua ameiacha.

Baada ya muda, meneja huyo kutoka nchini Chile alipata taarifa kutoka kwa dereva wa Taxi aliyokua ameipanda ambazo zilimfahamisha alikua amesahau hati yake ya kusafiria kwenye kiti cha nyuma cha gari hilo.

Pellgrini alipanda Taxi wakati akienda klabuni kujiunga na wachezaji wake kabla ya kupanda basi kubwa mbalo liliwapeleka kwenye uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya kuelekea nchini Ujerumani na ndipo alipojikuta hana hati ya kusafiria.

Hata hivyo Pellgerini, ilimlazimu kusubiri kwa dakika 35, na kujiunga na baadhi ya wachezaji waliokua wanasafiri kwa ndege ya pili iliyokua inaelekea nchini Ujerumani.

Magufuli Asema Atafuata Nyayo Za Marais Waliomtangulia
Jaji Lubuva Aziba Mwanya Mwingine Wa Wizi Wa Kura