Mwanasiasa wa Marekani ambaye pia alikuwa Spila wa Bunge katika kipindi cha miaka minne iliyopita, Nancy Pelosi wa Chama cha Democratic amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa Spika wa Bunge la Marekani.

Zoezi la kupiga kura lilifanyika Jumapili, Januari 3 ambapo matokeo yaliyopatikana ni 216-209.

Wabunge wawili wa Democratic walimpigia kura za Hapana na watatu wakionesha kutomkubali wala kumkataa.

Hivi sasa, Bunge la Marekani linakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukabiliana na mlipuko wa COVID – 19 na kufufua uchumi wa nchi.

Hii ni mara ya nne kwa Pelosi mwenye umri wa miaka 80 kushinda nafasi hiyo ya Spika wa Bunge la Marekani.

Songani: Tuna kazi kubwa kuing'oa Simba SC
Mazungumzo ya siri ya Trump yavuja