Makao makuu ya jeshi la Marekani, Pentagon, imelikataa pendekezo la kushangaza la Poland kwamba ingeliipa Marekani ndege zake za kijeshi kwa ajili ya kutumiwa na Ukraine, katika kile kinachotajwa kama ishara isiyo ya kawaida ya kutokubaliana wakati washirika wa muungano wa kijeshi wa NATO wakisaka kuwapa nguvu wanajeshi wa Ukraine bila kujihusisha moja kwa moja na uhasama na Urusi.

Msemaji wa Pentagon, John Kirby, amesema tangazo la Poland kwamba inakusudia kuwasilisha ndege zake 28 za kjeshi chapa MiG-29 katika kituo cha kijeshi cha Marekani cha Ramstein nchini Ujerumani, linazusha wasiwasi mkubwa kuhusiana na ndege za kijeshi kuondoka Marekani na kwenda kituo cha NATO na kuruka kwenye anga ambalo linawaniwa na Urusi katika mzozo wake na Ukraine.

Kirby aliongeza kwamba, wangeliendelea kushauriana na Poland na washirika wengine wa NATO juu ya suala hilo. Tayar, Urusi ilishatangaza kwamba kulisaidia jeshi la anga la Ukraine kutahisabiwa kama kushiriki vita na kutajibiwa kikamilifu.

Lakini pia Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliwashukuru viongozi wa Marekani na Uingereza kwa kupiga marufuku mafuta ya Urusi kuingia kwenye nchi zao. 

Zelensky aliita marufuku hiyo kuwa ni ishara kubwa kwa ulimwengu mzima, akisema sasa Urusi itapaswa kuheshimu sheria za kimataifa na kuacha kuanzisha vita ama ikose fedha.

Akizungumza na bunge la Uingereza, Zelensky alisema wakati alipoanza kuhutubia picha ya kuogofya zaidi ilikuwa ya watoto 50 waliouawa ndani ya siku 13 za vita, lakini wakati anamalizia walishafikia 52.

Rais huyo aliapa kutokusamehe wala kusahau maovu yaliyotendwa na wale aliowaita wavamizi na wakaliaji. Hata hivyo, Zelensky alitumia hotuba yake kutowa tena wito wa majadiliano ya kukomesha vita na Urusi. 

Dilunga kuikosa Berkane, Bocco, Mugalu, Kibu wapo FIT
Ahmed Ally: Tunajua umuhimu wa mchezo huu