Msanii wa nyimbo za kizazi kipya nchini, Diamond Platinumz ambaye amekuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mwanadada mfanyabiashara maarufu nchini Uganda, Zarina Hassan, penzi la wawili hao limeota nyasi mara baada ya Zari kuweka wazi hisia zake na kutangaza rasmi kuachana na kijana huyo.
Zari amechukua uamuzi huo katika siku ya Valentine maarufu kama siku ya wapendanao mnamo saa tatu na nusu usiku,
Kutumia kurasa wake wa instagram aliamua kurusha bomu lililomlipua Diamond pamoja na mashabiki wa wapenzi hao.
Kama ilivyo desturi katika sikukuu ya wapendanao wapenzi hupeana zawadi yakiwemo maua mekundu na mazuri ya waridi yanayoashiria upendo, lakini siku hiyo iliwaendea tofauti Zari na Daimond ambapo, Zari alipost ua jeusi mithili ya karatasi lenye ujumbe mzito lililoteketea na moto na kulisindikiza na ujumbe mzito ulioibua hisia za watu wengi.
Zari amebainisha kuwa sasa anasitisha rasmi mahusiano ya kimapenzi na Diaomd, lakini kwa kuwa kuna kitu kinawaunganisha basi wawili hao watabaki kuwa kama wazazi wa watoto wawili ambao ni Nillan na Tiffah.
Zari amesema kuwa ameshindwa kuvumilia tabia ya mwanaume huyo kushindwa kuwa mwaminifu katika mahusiano yao na kuwa anasikia mambo mengi yakiendelea mtandaoni mengine akiwa na ushahidi nayo.
Sasa Diamond Platinumz na Zarina Hassan sio wapenzi tena, ila watabaki kama wazazi.