Kocha Mkuu wa Klabu Bingwa nchini England ‘Manchester City; Pep Guardiola amekiri kwamba hajui jinsi kikosi chake kitakavyokuwa wakati wa kuanza kutetea mataji yao matatu msimu huu 2023/24.
Guardiola amezungumza na Kyle Walker huku kukiwa na nia ya kutoka kwa Bayern Munich, lakini beki huyo bado hajaamua juu ya mustakabali wake, wakati Bernardo Silva na Aymeric Laporte wote wanaweza kuondoka.
Hali ya kutokuwa shwari pale City ni wasiwasi kwa Guardiola, aliyepewa jukumu la kuipa historia tena timu hiyo.
“Tutaona tulichonacho mwisho wa dirisha la uhamisho, tutakuwa na timu gani.” alisema Guardiola.
“Kusema kweli sikufikiria kuwa kutakuwa na harakati hii, mambo mengi yanaenda kutokea. Ndio maana siwezi kujibu kwa sababu sijui.
“Nawatakia mema wachezaji wangu na bila shaka klabu inahusika na hilo pia. Nilizungumza na Kyle na kila kitu kiko sawa. Tutaona kitakachotokea. Siwezi kusema lolote kwa sababu bado nafikiria hilo.”
Man City wamemlenga beki wa kati wa Croatia, Josko Gvardiol, lakini hawajafikia thamani ya RB Leipzig, inayodhaniwa kuwa zaidi ya Pauni Milioni 80 na hadi sasa wamemnunua Mateo Kovacic pekee kutoka Chelsea kwa Pauni Milioni 25.
Riyad Mahrez anamfuata Ilkay Gundogan nje ya mlango, huku winga huyo akipata uhamisho wa Pauni Milioni 30 kwenda Al-Ahli, huku Joao Cancelo akirejea baada ya mzozo kati yake na Guardiola uliosababisha akopeshwe kwa Bayern Januari.
“Joao alikuwa muhimu sana kwetu siku za nyuma,” alisema Guardiola.