Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola amefanyiwa upasuaji wa dharura kutokana na maumivu makali ya mgongo na atakosa mechi mbili za Ligi Kuu England.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 alifanyiwa upasuaji na daktari Mireia Illueca, ambaye ni mtaalamu wa upasuaji wa uti wa mgongo mjini Barcelona na atabaki huko hadi atakapopata nafuu.
Guardiola amekuwa akisumbuliwa na mgongo kwa muda mrefu na alipanga kufanyiwa upasuaji, hivyo timu itakuwa chini ya kocha msaidizi Juanma Lillo.
Lillo ataiandaa timu kuelekea mechi mbili za ligi dhidi ya Sheffield United na Fulham zitakazopigwa kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa mwezi ujao.
Pia, Guardiola atakosa utambulisho wa winga mpya Jeremy Doku aliyesajiliwa kutoka Rennes kwa Pauni 55 milioni, huku akiendelea kusaka kiungo mwingine wa kati.
Man City inatarajiwa kutangaza mkataba mpya wa Bernardo Silva baada ya kufikia makubaliano na kiungo ambaye ilisemekana aliku- wa anataka kuondoka.
Kufuatia kukosekana kwa Guardiola hofu imeibuka miongoni mwa mashabiki wa timu hiyo juu ya mwendelezo wa kikosi chao kufanya vizuri.
Kufuatia upasuaji huo wafanyakazi wa Man City wamemtakia heri na wanatarajia kumuona akirejea Manchester kuendelea na majukumu yake.
Taarifa ya klabu iliripoti baada ya upasuaji: “Lillo ni mtu anayeheshimika katika timu na Guardiola anamchukulia kama mshauri wake mzZuri. Wawili hawa walicheza pamoja kabla ya kustaafu kucheza soka.”
Lillo, 57, ameitumikia Man City kwa miaka miwili akiwa kocha msaidizi tangu 2020 na kabla ya hapo alikuwa ni Mikel Arteta.