Kocha wa Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City, Pep Guardiola, ameamua kukutana uso kwa uso na kiungo wa West Ham United, Declan Rice ikiwa ni sehemu ya kumshawishi kutua klabuni hapo na kuachana na mpango wa kwenda Arsenal.

Hii ni baada ya West Ham United kukataa ofa ya kwanza ya Manchester City ambayo walipeleka kiasi cha Pauni 80m sambamba na fedha ya ziada Pauni 10m.

Wakati Man City wakipeleka ofa hiyo, Arsenal wameshapeleka ofa mara tatu kwa West Ham na zote zimekataliwa.

Kutokana na hilo, hivi sasa vita imebaki kwa Man City na Arsenal juu ya kumuwania nyota huyo wakati West Ham United wakisema dau la Rice ni pauni 100m.

Imeelezwa kuwa, Guardiola alikutana na Rice na kuzungumza naye uso kwa uso kumshawishi kutua ndani ya kikosi hicho na sio kwenda timu nyingine.

Guardiola anapambania dili hilo hasa baada ya kuondoka kwa Ilkay Gundogan.

Inaelezwa kuwa, hata Mikel Arteta alishajaribu kumshawishi Rice na kumuhakikishia atakuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi chake, lakini hadi sasa bado hakijaeleweka.

Francis Baraza aiweka njia panda Geita Gold
Gamondi kutua Dar na wasaidizi wake