Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema anafurahia maisha ya klabu hiyo japo anaendelea kuzungumzwa tofauti katika vyombo vya habari kutokana na usajili wa nguvu alioufanya katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Guardiola anaandamwa na vyombo vya habari, kwa kuhisiwa huenda akashindwa kufikia malengo ya kufanya vyema msimu huu, hali ambayo inaweza kumuingiza katika majaribu ya kufukuzwa kazi klabuni hapo.

Guardiola amewaambia waandishi wa habari katika mkutano uliokua unazumngumzia mchezo wa ligi ya England dhidi ya Everton utakaochezwa leo katika dimba la Etihad mjini Manchester, kwa kusema hana shaka na kazi yake.

Meneja huyo kutoka nchini Hispania amesema anafurahia kufanya kazi kwa Pesha inayotoka katika vyombo vya habari, na hadhani kama atashindwa kama inavyoelezwa kila kukicha.

“Ninarudia kusema tena kama nilivyosema msimu uliopita, ninatarajia matokeo mazuri na sidhani kama tutashindwa kufikia lengo, nafuatilia kinachozungumzwa na kuandikwa katika vyombo vya habari. Kwa kweli yote hayo hayaninyimi usingizi kabisa.” Amesema Guardiola

“Hakuna anaejua ninachotarajia kukifanya msimu huu zaidi yangu mimi ambaye ndio muhusika, ninashauri baadhi ya waandishi fanyeni kazi zenu kiweledi na sio kumshupalia mtu mmoja kwa kuomba afanye vibaya.

“Tangu nimekubali kuja hapa (Man City), nimekua sijali kilachoandikwa/kuzungumzwa kuhusu mimi. Na jambo hilo ninakiri kwa kusema, ninalimudu sana.

“Nilipokua Bayern, nilitwaa ubingwa wa Bundesligas mara tatu mfululizo, nikafika nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mara tatu. Na kisha niliondoka na kuja hapa, Najua naweza kulimudu hili linalonikabili kwa sasa.

Guardiola amekua meneja anaetarajiwa kufanya maajabu katika ligi ya nchini England tangu alipoanza kukifundisha kikosi cha Man City msimu uliopita, na anafuatiliwa kwa ukaribu na vyombo vya habari, hasa baada ya kushindwa kufikia lengo la kutwaa ubingwa.

Msukuma amkumbuka Nape sakata la Bombardier
Dkt. Shein afuta kero ya barabara Kijitoupele, awafungukia waliombeza