Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola ametoa angalizo kwa mashabiki wa timu hiyo kwa kusema haitakuwa rahisi kuwafunga wapinzani wao Arsenal kesho Jumapili (Oktoba 08).

Man City ambao wanaongoza kileleni mwa msimamo wa Premier kesho Jumapili (Oktoba 08) watakuwa wageni wa Arsenal katika mechi ya ligi itakayopigwa Uwanja wa Emirates, jijini London.

Guardiola ataingia kwenye mechi hiyo akiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa na Arsenal kwenye Ngao ya Jamii mapema kabla ligi haijaanza.

Akizungumzia mechi hiyo, Guardiola alisema: Nina hisia kwamba haitakuwa jambo rahisi kuwafunga Arsenal. Tunaenda kwenye mechi hii kucheza mchezo wetu.

Nitawategemea hawa watu bila masharti kushinda au kutoshinda, kwa sababu na vipindi vya mazoezi vilivyo, mawazo waliyonayo na wanathibitisha hilo,” alisema Guardiola.

Lewandowski hatarini kuikosa El Clasico
Minziro: Nitapambana hadi kieleweke TZ Prisons