Kocha Pep Guardiola anaamini ni ishara nzuri ikiwa wachezaji wake wa Manchester City watakuwa na hasira ya kuachwa nje ya kikosi cha kwanza.
Jeremy Doku alifunga na kutoa asisti nne katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Bournemouth Jumamosi (Novemba 06).
Winga huyo alikuwa kwenye benchi katika ushindi wa juma lililopita dhidi ya Manchester United, huku Jack Grealish akianza, lakini majukumu yalibadilishwa wakati wa mchezo wa Jumamosi.
“Nataka Jack (Grealish) awe na hasira na nataka acheze vizuri,” alisema Guardiola.
Na kisha Doku kuwa na hasira kwamba hajacheza mechi mbili zilizopita. Hii ndiyo njia ya kudumisha uthabiti katika kiwango hicho.”
Huku City ikisonga kileleni mwa Ligi Kuu England Jumamosi ikiipita Tottenham Hotspur pointi moja ambapo jana Jumatatu (Novemba 06) ilikubali kupoteza dhidi ya Chelsea iliyoshinda 4-1, na mchezaji wa Kimataifa wa Ubelgiji, Doku aliyesajiliwa kwa Pauni milioni 55.4 kutoka Rennes majira ya joto, ameimarika haraka akifunga mabao matatu katika mashindano yote.
Doku mwenye umri wa miaka 21, anapambania namba na Grealish, ambaye hakutumika kamamchezaji wa akiba wikiendi na bado hajafunga bao kwenye ligi msimu huu.
Guardiola alisema: “Kama vile Jeremy na Jack wanavyofanya na ninaweza kuwachezesha wote wawili kwa wakati mmoja, lakini lazima wanishawishi kwenye mazoezi.
Jinsi (Grealish) alivyocheza pale Old Trafford, ili kutupa utulivu zaidi na nguvu zaidi katika nafasi hiyo, ilikuwa uamuzi kwetu.
“Tunahitaji kila mtu. Kuna michezo mingi na kila mtu anatakiwa kushindana.
“Basi tutashinda michezo na mtafurahi na kila mtu atafurahi. Hiki ndicho tunachopaswa kufanya.”
Man City itawakaribisha mabingwa wa Uswisi Young Boys katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baadae leo Jumanne (Novemba 06).