Jina la Pep Guardiola limeendelea kuwa katika baadhi ya vyombo vya habari nchini England na kwingineko kuhusu mipango ya usajili wa majira ya kiangazi, licha ya suala la mlinda mlango kutoka nchini Chile na FC Barcelona Claudio Bravo kufahamika.

Gazeti la The Manchester Evening limeripoti kuwa, meneja huyo kutoka nchini Hispania bado hajafurahishwa na mwenendo wa usajili wake hususan katika safu ya ulinzi, licha ya kukamilisha usajili wa beki John Stones kwa kiasi cha Pauni milioni 47.5 majuma mawili yaliyopita.

Beki wa klabu bingwa nchini Italia Juventus FC, Leonardo Bonucci anatajwa kuwa katika mipango ya meneja huyo ya kuimarisha safu ya ushambulia ya Man City.

Hatua ya kutokuwepo kwa nahodha Vincent Kompany ambaye ni majeruhi pamoja na Eliaquim Mangala ambaye yupo katika harakati za kutaka kuuzwa kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, imekua ikiibua maswali kwa Guardiola kuhusu safu yake ya ulinzi ambayo inapaswa kuwa bora ili kutimiza malengo ya kutwaa ubingwa mwishoni mwa msimu huu.

Tayari Man City wameshatumia karibu kiasi cha Pauni milioni 150 kwa kufanya usajili wa Stones, Ilkay Gundogan, Leroy Sane, Nolito, Oleksandr Zinchenko, Marlos Moreno pamoja na Gabriel Jesus ambaye ataelekea Etihad Stadium mwezi januari mwaka 2017.

Kwa sasa klabu hiyo ya mjini Manchester inaangalia uwezekano wa kumsajili mlinda mlango wa FC Barcelona Claudio Bravo kwa kiasi cha Pauni milioni 14 kama mbadala wa Joe Hart, ambaye wakati wowote ataondoka na kujiunga na klabu itakayofikia dau litakalo tangazwa.

Pau López Sabata Kuuwahi Mchezo Wa Kesho?
Diego Simeone: Sikuwahi Kusema Hadharani Ninataka Kuondoka