Klabu ya Everton inajipanga kuwasilisha ofa ya kutaka kumsajili mlinda mlango kutoka nchini England na klabu ya Man City, Joe Hart Baada ya kuonekana hana nafasi katika kikosi cha kwanza cha meneja Pep Guardiola.

Everton wanajipanga kufanya hivyo na wanaamini dili hilo litakamilishwa kabla ya dirisha la usajili halijafungwa mwishoni mwa mwezi huu.

Gazeti la Daily Mail limeripoti kuwa, Everton walipata nguvu ya kuamini huenda wakafanikiwa kumpeleka Hart Goodison Park, kufuatia mazingira yaliyoonekana wakati wa mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya England ambapo mlinda mlango huyo chaguo la kwanza kwa upande wa timu ya taifa alikalishwa benchi.

Taarifa za kutoka ndani ya Man City, zineeleza kuwa, Hart alikua amejumuishwa katika kikosi ambacho kingeanza dhidi ya Sunderland, lakini dakika chache kabla ya mchezo jina lake liliondolewa kwenye orodha.

Alipoulizwa Guardiola mara baada ya mchezo huo, alisema Hart hakuwa katika hali nzuri na ndio maana alifanya maamuzi ya kumpumzisha, jibu ambalo lilionesha kupokelewa kwa hisisa tofauti na waandishi wa habari.

Hata hivyo inaelezwa kwamba huenda Guardiola akatuma ofa ya kumsajili mlinda mlango wa mabingwa wa soka nchini Hispania FC Barcelona  Claudio Bravo, ili kuimarisha nafasi ya ulinzi wa lango la kikosi chake.

Arsene Wenger: Tulikosa Wachezaji Wenye Uzoefu
Wapinzani Zambia walia kuibiwa kura, Rais Lungu aongoza matokeo ya awali