Klabu ya Manchester City imethibitisha kukamilisha mazungumzo ya mkataba na kocha Pep Guardiola kuwa meneja mpya wa klabu hio kuanzia msimu ujao wa 2016/17.

Kupitia waraka rasmi wa klabu, Manchester City imesema Guardiola amepewa mkataba wa miaka mitatu kuwanoa mabingwa hao wa zamani wa Uingereza wenye uchu na matarajio makubwa ya mafanikio.

Man City imetangaza kuwa kutokana na heshima kwa meneja wao wa sasa, Pellegrini imeona ni vyema kuweka mambo wazi kuondoa mzigo na presha ya tetesi.

Hivyo wamethibitisha mapema, Pellegrini ataihama klabu hiyo mwishini mwa msimu huu na wanamtakia mafanikio mema.

 

Sserenkuma Akamilisha Mipango Ya kucheza Uganda
Ma-MC, Wapishi, Kumbi za Harusi kuanza kulipa kodi