Meneja wa Klabu Bingwa nchini England Manchester City, Pep Guardiola, amesema mchezo kati ya timu yake dhidi ya Arsenal utakuwa kama Fainali na ndiyo utakaoamua ubingwa wa Ligi Kuu nchini humo ‘EPL’ msimu huu 2023/24.

Guardiola alitoa kauli hiyo baada ya kikosi chake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Leicester City na kuzidi kuikaribia Arsenal katika mbio za kuwania ubingwa huo, huku alama 4 zikizitenganisha timu hizo katika nafasi ya kwanza na yapili.

Katika msimamo wa ligi hiyo Man City inashika nafasi ya pili ikiwa na alama 70 wakati Arsenal ikiongoza ligi ikiwa na pointi 74, timu zote zikicheza michezo 30.

Man City itavaana na Arsenal katika mchezo ujao wa Ligi Kuu ya England utakaochezwa Jumatano Juma lijalo katika Uwanja wa Etihad, Manchester nchini England.

Guardiola amesema mchezo huo utakuwa kama Fainali kwani kikosi chake kikipoteza mchezo huo kitakuwa kimekamilisha mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England.

“Kama nilivyosema katika mikutano iliyopita, ni ushindi, ushindi, ushindi. (Arsenal) wamekuwa na mwendo mzuri hadi sasa msimu huu,” amesema.

Kocha huyo amesema haamini kama Arsenal itapoteza alama nyingi katika michezo iliyosalia msimu huu 2022/23

“Ni muhimu kwetu kufika katika mchezo kwa kushinda mchezo dhidi ya Leicester na ni Fainali dhidi yao katika mchezo ujao wa Ligi Kuu ya England.

Kabla ya haijavaana na Man City, Arsenal inayonolewa na Meneja kutoka nchini Hispania Mikel Arteta itacheza na Southampton siku ya Ijumaa (April 21).

Mkataba upanuzi Mkongo wa Taifa mawasiliano wasainiwa
Ajali ya basi yauwa 11 wakitoka kwenye mazishi