Nahodha na beki wa klabu ya Arsenal Per Mertesacker yu njiani kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia The Gunners yenye maskani yake makuu kaskazini mwa jijini London.

Kituo cha televisheni cha Sky Sports kimeripoti kuwa, uongozi wa Arsenal umekamilisha sehemu ya mazungumzo na beki huyo kutoka nchini Ujerumani, na wakati wowote kuanzia sasa atakamilisha mpango wa kusaini mkataba mpya.

Sky Sports wameongeza kuwa, Arsenal wamechukua jukumu la kuendelea kufanya kazi na Mertesacker ambaye mkataba wake ulikua unafikia kikomo mwishoni mwa msimu huu, baada ya kuona kuna umuhimu wa kupata huduma yake kwa kipindi kingine.

Wakati mpango wa mkataba mpya ukiandaliwa, beki huyo mwenye umri wa miaka 32, bado anaendelea kukaa nje ya uwanja kufuatia majeraha ya mguu aliyoyapata mwanzoni mwa msimu huu, hali ambayo imemsababishia kushindwa kukosa michezo ya ligi na michuano mingine ambayo Arsenal wanashiriki.

Mertesacker alikua chaguo la kwanza katika safu ya ulinzi ya Arsene Wenger msimu uliopita, na alicheza michezo 36.

Kwa ujumla ameshacheza michezo zaidi ya 200 tangu aliposajiliwa klabuni hapo mwaka 2011 akitokea Werder Bremen, kwa ada ya uhamisho wa Pauni milioni 8.

Video: Airtel yazindua Kliniki ya Rising Stars
Maisha Ya Camp Nou Yamchosha Arda Turan