Beki kutoka nchini Ujerumani, Per Mertesacker amesema anaamini ilikuwa ni miujiza kwa Arsenal kumaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Engoland msimu uliopita.

Arsenal waliwazidi kete wapinzani wao wa kaskazini mwa jijini London Tottenham Hotspurs na kushika nafasi ya pili siku ya mwisho kabisa ya msimu, licha ya kuwa na tofauti ya point 10 dhidi ya Leicester City walioibuka mabingwa.

Mertesacker, ambaye anataraji kutangazwa kuwa nahodha mpya wa kikosi cha The Gunners kufuatia kustaafu kwa Mikel Arteta anaamini hatua hiyo kwa Arsenal ilikuwa na bahati kubwa.

“Kwa namna ambavyo msimu uliopita ulienda, tulikuwa ni wenye bahati kubwa kumaliza nafasi ya pili,” aliliambia gazeti la The Sun

“Mambo yalibadilika siku ya mwisho na hali hiyo ikawa kama kiujiza kwetu kumaliza nafasi ya pili.”

“Kilichotufedhehesha ni kwamba Leicester walitumia vizuri sana udhaifu wa vilabu vikubwa kujichukulia pointi lakini sisi tulishindwa.”

Huku zikiwa zimebaki wiki tatu kabla ya kuanza kwa msimu mpya, Arsenal mpaka sasa wamesajili mchezaji mmoja tu mwenye jina kubwa ambaye ni Granit Xhaka kabla ya kukutana na Liverpool August 14.

Na Mertesacker anaamini kwamba usajili uliofanywa na wapinzani wao utaleta ushindani mkubwa kuelekea msimu mpya wa ligi hasa kwa timu yake ya Arsenal.

“Hii itakuwa changamoto kubwa kwetu, kuhakikisha tunapambana na timu zote bora ambazo zilimaliza nyuma yetu,” aliongeza.

“Bila shaka, timu hizo kubwa zitakuwa imara zaidi msimu huu. Hicho ndivyo tunavyotaraji kuona msimu mpya utakapoanza huku kukiwa na wachezaji wengi wapya.

“Usajili mwingi umefanyika, na kamwe haitaokuwa rahisi kwetu msimu huu, hasa kutokana na usajili uliofanywa na wenzetu.”

FC Barcelona Wakubali Kumsajili Kevin Gameiro
Diwani apambana na Majambazi wenye bunduki, apishana na risasi