Wakati wa tamasha la Netflix Joke huko Los Angeles, Davidson alizungumza juu ya uhusiano wake na Kanye, ikiwa ni pamoja na uvumi uliosambaa mapema Januari kuwa Kanye West alieneza taarifa za uongo kuwa Davidson ni muathirika wa UKIMWI.
Licha ya Kanye kumkandamiza kwa maneno na shutuma nzito, Pete Davidson, yeye hajayafanya matendo ya Ye kama suala la kumuumiza au kuzalisha chuki dhidi yake na ameamua kuitumia shutuma ya kuwa muathirika wa virusi vya ukimwi kama utani kwenye onyesho lake kama sehemu ya kuwafurahisha wahudhuriaji.
Katika utani huo aliwaambia kwamba “alikuwa na hofu ya kuwa na UKIMWI mwaka huu,” na kwamba alienda kwa daktari kwa ajili ya kuchunguzwa, kwa kuwa Ye ni “Genius,” kwa namna fulani.”
Davidson pia alidhihaki jinsi Ye alivyomfanyia mke wake wa zamani Kim Kardashian, kwa kumtumia mama huyo wa watoto wake wanne lori lililojaa maua ya waridi.
Davidson alilinganisha matendo ya mwanamuziki huyo na yale ya Robin Williams katika filamu ya Mrs. Doubtfire, ya mwaka 1993, alipovalia kama mfanyakazi wa nyumbani ili kutumia wakati mwingi na watoto wake.
“Ni mimi pekee kwa siri mwenye matumaini ya Kanye kuwa kama mrs doubtfire ?” Davidson alitania.
Wakati huo huo Davidson alimgusia mwanamuziki Jack Harlow aliyeshirikishwa kwenye moja ya nyimbo za Ye inayopatikana kwenye album yake Donda 2, miezi michache tu baada ya kutoka kubarizi na mchekeshaji huyo Januari 2022 kitendo ambacho Davidson anadai kuwa hakikumuumiza badala yake kilimuacha na mshangao kwa namna fulani.
West aliwahi kuishutumu familia ya Kardashian kwa kutompa anwani ya sherehe ya kuzaliwa kwa binti yake Chicago, kabla ya kuthibitisha kuwa alihudhuria baada ya kushiriki video akielezea tukio hilo.
West pia amedai Kardashian hakuwaruhusu watoto wao kuhudhuria Ibada ya Jumapili mwezi Machi, kabla ya Kardashian kumuuliza kwenye Instagram “kuachana na simulizi hizo.”
Pete Davidson kwa sasa ndie mpenzi mpya wa Kim Kardashian baada ya Kim kuachana na Kanye West.