Wasanii maarufu wa Hip-hop, nchini Nigeria Peter na Paul Okoye, wanaounda kundi la Psquare kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya vizuri katika muziki wao nchini humo wamevunja mkataba wa kundi hilo mara baada ya Peter Okoye kumtaka mwanasheria wao Festus, Kuvunja kundi hilo.

Peter amesema kuwa inaonekana kuwa ndugu yake Paul hayupo tayari kuendelea kufanya kazi na yeye kwani ameweza kusitisha ziara yao ya US bila ya kuweka sababu yeyote.

Ameongeza kuwa, Paul amekuwa akimtukana mkewe na watoto wake kupitia mitandao ya kijamii na kusema familia yake imekuwa ikitumiwa ujumbe uliokuwa ukiwatishia maisha.

Hivyo msanii huyo ambaye alikuwa anaunda kundi hilo pamoja na pacha wake Paul Okoye ameweka wazi kuwa hawezi  kumsaliti mke wake pamoja na watoto wake kwa ajili ya kundi hilo na kutaka kuvunja kundi hilo ili kuokoa familia yake ambayo inaingizwa katika matatizo kutokana na umoja wake na ndugu zake Paul na Jude.

Pia Peter ameamua  kumshitaki kaka yake ambaye pia ni meneja wake, Jude kwa kumtishia kumuua kwa bastola yeye na mke wake.

Mr.P ambaye ni Peter amesema kuwa kwa sasa anachotaka ni kujiondoa katika kundi la  Psquare na kuvunja mkataba na ndugu yake Paul Okoye.

Si mara ya kwanza kwa wawili hao kuripotiwa  kwamba wamevunja kundi hilo, mwaka jana ilikuwa hivyo lakini wadau mbalimbali wa muziki duniani waliingilia kati na kumaliza tofauti zao lakini hii ya sasa inawaweka mashabiki njia panda.

 

Dortmund kuivaa Real Madrid leo
Wafuasi wa NASA kuandamana leo Kenya