Mwananasheria wa Chadema, Tundu Lissu na mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chadema, Mchungaji wametoa mtazamo wao kwa nyakati tofauti kuhusu uamuzi wa  aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk. Wilbroad Slaa kukitosa chama hicho.

Wanachama hao wa Chadema ambao hivi karibuni wameonekana kumsapoti kwa nguvu mgobea urais wa Chadema ambaye walimtuhumu kuwa fisadi akiwa CCM, Edward Lowassa wamepinga na uamuzi pamoja na sababu alizozitoa Dk. Slaa katika mkutano wake na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

Akiongea na kituo kimoja cha radio jijini Dar es Salaam, Tundu Lissu alipinga maelezo yaliyotolewa na Dk. Slaa na kudai kuwa yeye ndiye wa kwanza kutoa wazo la kumkaribisha Dk. Slaa kwenye chama hicho.

“Kamati kuu ilimpitisha mwezi January ikathibitisha tena mwezi April, ilipofika mwezi wa Tano ni Dk Slaa ndiye aliyeanzisha tena mazungumzo ya kumleta Lowassa ndani ya Chadema,” alisema.

“Yeye anasema Gwajima alikuwa mshenga, hajasema mposaji ni nani, nani aliyemuendelea Gwajima kumwambia kwamba tunamtaka Lowassa, sio mwingine ni huyo Dk. Slaa,” alisisitiza.

Mwanasheria huyo wa Chadema alidai kuwa chanzo cha Dk. Slaa kugeuka mpango aliokuwa akiusuka yeye ni mtazamo tofauti alioupata kwa mkewe Josephine ambaye alizua ugomvi mkubwa.

“Kilichoharibika ni first lady, mama alikataa,” alisema na kufafanua kuwa siku ambayo Kamati Kuu ya Chadema ilimpokea Edward Lowassa katika chama hicho mkewe Josephine alimtupia mabegi nje na kusababisha alale ndani ya gari.

Kwa upande wa Mbunge wa Iringa Mjini anayemaliza muda wake, Mchungaji Peter Msigwa, alitumia ukurasa wake wa Twitter kutoa mtazamo wake kuhusu uamuzi wa Dk. Slaa.

“Kwenye  mapambbno  haijalishi  mateka  amesema  nini  kwa  adui,  ni  mbele  kwa  mbele, the move is unstoppable ! Wish you well Dr!,” Msigwa alitweet jana.

“Huyo mla mihogo anayeweza kulipia live TV coverage atasifiwa sana wiki HII na uhuru , mzalendo habari Leo pamoja na tbc,” inasomeka tweet nyingine ya  Mchungaji Msigwa.

Jana, Dk. Slaa alitangaza kustaafu siasa za vyama baada ya kutoridhishwa na uamuzi wa Chadema kumpokea Lowassa bila kutimiza masharti aliyowapa awali huku akisisitiza kwa kutoa vielelezo kuwa mgombea wa Chadema ni fisadi mkubwa aliyejinufaisha kupitia sakata la Richmond na Dowans.

 

 

 

Lennon Achukuliwa Jumla Goodson Park
Lil Ommy Wa Times Fm Aachia Toleo Jipya La ‘The Playlist Magazine’ Bure