Aliyekua mlinda mlango mshahuri wa klabu ya Man Utd, Peter Bolesław Schmeichel ni miongoni mwa waliowasilisha maombi ya kutaka kukinoa kikosi cha klabu ya Leicester City ambacho kitashiriki michuano ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza, msimu wa 2015/16.

Taarifa zilizofanyiwa uchunguzi na kituo cha televisheni cha Sky Sports na kubainika kuwa mlinda mlango amewasilisha maombi ya kutaka kuwa meneja wa klabu hiyo, zimewashtua mashabiki wengi.

Schmeichel, ambaye pia aliitumikiua timu ya taifa ya nchini kwao Denmark kuanzia mwaka 1987-2001, hajawahi kuwa meneja wa klabu yoyote tangu alipotangaza kustahafu soka mwaka 2003 akiwa na klabu ya Man City.

Kasper Schmeichel, mtoto wa mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 51, ni miongoni mwa wachezjai wanaunda kikosi cha klabu ya Leicester City. Hivyo, kama baba yake atakubaliwa kupewa ajira klabuni hapo, watakuwa karibu na kuongeza hamasa ya kung’arisha ndoto za mwanae anapokua golini.

Naye kocha wa timu ya taifa ya jamuhuri ya Ireland, Martin O’Neill anatajwa katika harakati za kuwania kibarua cha kukinoa kikosi cha klabu ya Leicester City, ambayo aliisaidia kupanda daraja na kucheza ligi kuu ya soka ya Uingereza mwaka 1996.

Mchaka mchaka wa kumsaka mkuu wa benchi la ufundi huko King Power Stadium, umetokana na hatua za kutimuliwa kazi kwa aliyekua meneja klabuni hapo Nigel Nigel Pearson.

Van Persie atuwa Kwa mbwembwe Istanbul
Sterling Ashinda Vita, Liverpool Wakubali Kumuachia