Aliyekua kiungo wa klabu za Arsenal na Chelsea zote za nchini England, Emmanuel Laurent Petit, ameshindwa kujizuia kuficha siri muhimu katika maisha yake ya soka na hatimae amejikuta akiitangaza hadharani.

Petit, ambaye kwa sasa anajishughulisha na masula yake binafsi pamoja na uchambuzi wa soka katika kituo cha televisheni cha Canal Sports cha nchini kwao, amesema aliwahi kuhitajika kwenye klabu ya Man Utd lakini alikataa kuitikia wito huo.

Petit amesema baada ya kukaa kwa muda wa miaka sita jijini London na kuonyesha uwezo mkubwa kisoka katika klabu ya Arsenal, alipata ofa kutoka FC Barcelona na aliitikia wito huo kutokana na hitaji lake la kutaka kucheza soka nchini Hispania.

Amesema baada ya kuona mambo yanakua magumu nchini Hispania alitamani kurejea nchini England, na ndipo Sir Alex Ferguson alipoonyesha dhamira ya kutaka kumsajili, lakini alikataa na kuelekea Chelsea ambapo alicheza michezo 75 bila ya kupata mafanikio.

Kutokana na hali hiyo Petit anadai alijuta kufanya maamuzi ambayo yalikua sio sahihi katika soka lake, kutokana na kuamini kwamba endapo angejiunga na Man Utd huenda angemaliza medani ya soka kwa mafanikio ya kihistoria.

Petit alitangaza kustahafu soka akiwa na klabu ya Chelsea mwaka 2004 kufuatia majeraha ya goti ambayo yalimsumbua kwa muda mrefu.

Niko Kovac Afungashiwa Virago Croatia
Magufuli Alia Na Posho, Ataja Mawaziri Wake Kwa Sifa