Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imesema Petroli inayopitia bandari ya Dar es Salaam imepungua kwa Shilingi 59, huku ruzuku ya mafuta inayotolewa na Serikali katika eneo hilo ikiondolewa kwa mafuta ya Dar es Salaam na bei ya Petroli inayopitia Mtwara ikipungua kwa Shilingi 92 kwa mwezi Desemba na Tanga ikiongezeka kwa Shilingi 9.
Hatua hiyo, itafanya bei ya mafuta ya Petroli kwa upande wa Dar es Salaam kushuka hadi Shilingi 2, 827 kutoka Shilingi 2,886 iliyokuwa i ikitozwa Novemba, 2022 na kulingana na ukomo wa bei ya mafutaya mwezi uliopita, bei ya petroli kwa Tanga imefikia Shilingi 2,815 kutoka Shilingi 2,806 na Mtwara Petrol ikiwa Shilingi 2,825 kutoka Shilingi 2,917.
Aidha, bei ya dizeli ya rejareja kwa Dar es Salaam imeongezeka kwa Shilingi 278, Tanga Shilingi 422 na Mtwara Shilingi 416 na EWURA inasema ili kukabiliana na athari za ongezeko la bei za mafuta nchini kutokana na shughuli nyingi za kiuchumi kutumia mafuta ya Dizeli, Serikali imetoa ruzuku kwa bei ya Desemba 2022.
Kutokana na Ruzuku hiyo, bei ya mafuta ya dizeli imepungua kwa Shilingi 83 kwa lita, Shilingi 247 na Shilingi 243 kwa Dar es Salaam, Tanga na Mtwara na sasa Dizeli itauzwa kwa Shilingi 3,247 kutoka Shilingi 3,052 ya mwezi Novemba kwa upande wa Dar es Salaam huku Tanga Dizeli ikiwa ni Shilingi 3,496 kutoka Shilingi 3,249 na Mtwara kwa Shilingi 3,512 kutoka Shilingi 3,269.