Beki wa pembeni na nahodha wa mabingwa wa soka nchini Ujerumani, Philipp Lahm amesema angependa watwae mataji matatu kabla ya meneja wao kutoka nchini Hispania, Pep Guardiola hajaondoka mwishoni mwa msimu huu.

Guardola atamaliza mwaka wake wa tatu akiwa na klabu hiyo ya mjini Munich ifikiapo mwishoni mwa msimu huu ili akatafute kibarua nchini England, lakini Lahm anasema ameipa Bayern kipindi kizuri.

Lahm alisema kwamba licha ya kushuhudiwa Pep aiondoka, lakini wanajianda kufanya kazi chini ya kocha mwingine mahiri wakati Carlo Ancelotti atakapowasili.

“Nimewahi kuwa chini ya makocha mahiri Ujerumani kama vile; Ottmar Hitzfeld, (Felix) Magath, Jupp Heynckes na wale wa kigeni kama Lois Van Gaal, Pep Guardiola  na sasa anakuja mwingine, Carlo Ancelotti ambaye amewahi kutwaa mataji ya Klabu Bingwa Ulaya misimu mbalimbali,” alisema Lahm

“Hivyo basi nikiangalia mbeleni, naona kuna mafanikio mengine tukiwa chini ya Pep. Kila mmoja anamfahamu mwenzake vyema na tunafurahi kucheza chini yake,” aliongeza nyota huyo.

Alisema, tangu ameanza kucheza soka akiwa na miaka sita na kisha akawa mchezaji mkubwa, amekuwa akishuhudia makocha wakija na kuondoka nahiyo akasema kuwa ni sehemu ya soka linavyokwenda.

John Terry Ategemea Miujiza Stamford Bridge
Leicester City Inakaribia Kumnasa Amartey