Kwa mara ya kwanza kiungo mpya wa mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich Philippe Coutinho amezungumzia maisha anayoishi katika jiji la Munich.

Kiungo huyo alijiunga na mabingwa hao wa Bundesliga kwa mkopo wa msimu mmoja, akutokea FC Barcelona ya Hispania kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi.

Coutinho amedai maisha ya FC Bayern Munich kwake yamekuwa kama familia zaidi, kuliko hata kwenye klabu mbili alizopita huko nyuma, Liverpool na Barcelona.

Mchezaji huyo kutoka nchini Brazil, ameonekana kutulizana kwa haraka kwenye maisha ya Ujerumani, ambapo ameshacheza michezo mitatu ya Bundesliga katika kikosi hicho hadi sasa.

Mwenyewe alisema anaona Allianz Arena pamekuwa na mapokezi mazuri kwake kuliko hata muda wake wa miaka mitano aliyodumu kwenye kikosi cha Liverpool na kucheza zaidi ya michezo 200.

“Ndani ya siku hizi chache zilizokuwa hapa na kuonyeshwa mazingira, nimekutana na wachezaji wenzake na makocha. Kila siku najisikia vizuri sana, nina furaha. Bayern pamekuwa kama familia zaidi kuliko klabu zangu za zamani,” alisema Coutinho mwenye umri wa miaka 27.

FC Bayern Bayern walimsajili Coutinho kwa Pauni milioni 7.6 kwa mkopo wa msimu mzima, na walikubali kumlipa mishahara yake yote kwa kipindi hicho atakachokuwa akikipiga kwenye kikosi chao.

Hata hivyo Coutinho almanusura angerejea Liverpool, kufuatia uongozi wa FC Barcelona kumtaka meneja wa The Reds Jurgen Klopp kumsajili kwa mkopo, lakini aligoma kufanya hivyo.

Kocha Klopp alikiri kwamba kikosi chake kiliamua kuachana na Coutinho na wakati walipopewa nafasi ya kumrudisha Anfield staa huyo, akisema kwamba amemshauri mchezaji huyo aende Bayern ndiko kunakomfaa zaidi. Klopp alisema: “Nilimwambia Bayern patakuwa bora zaidi kwake.

Ni mchezaji wa kiwango cha dunia na hakika ni usajili bora kwa Bayern na Bundesliga.”

Chris Brown kuwa 'Bestman' harusi ya Davido
Video: Meya Kinondoni awakingia kifua wauza mihogo Coco