Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu, Dkt Jakaya Kikwete amefungua mkutano wa kamati kuu ya CCM kwenye ukumbi wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. Ambapo Dkt Kikwete ameeleza kuwa ajenda ya mkutano huo ni yeye kun g’atuka na kumpa nafasi Rais wa awamu tano, Rais John Pombe Magufuli

1

Katibu mkuu wa CCM, Abdallahaman Kinana akimpokea mwenyekiti mtarajiwa wa CCM, Rais John Pombe Magufuli akiwasili kwenye mkutano wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma.

 

IMGS7208Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakiimba  wimbo wa CCM katika kikao cha  Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichofanyika mjini Dodoma Julai 21, 2016.

 

IMGS7221Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Pombe Magufuli akiteta na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar,  Dkt. Ali Mohamed Shein katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM uliofanyika mjini Dodoma Julai 21, 2016.

IMGS7232
Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete wakati alipofungua mkutano wao mjini Dodoma Julai 21, 2016.
IMGS7252
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Pombe Magufuli na Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein . Kulia ni Makamu Mwenye kiti wa CCM, Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Trump Asema Yeye ni Sauti ya Wamarekani
Stamina Aisifu Couple ya jux na Vee Money kwa Kumpa Ushirikiano katika Wimbo Wake.