Mwimbaji wa Bongo Flava mwenye mashabiki wengi Tanzania, Ali Kiba yuko jijini Nairobi tayari kwa kuanza kazi ya kurekodi msimu mpya wa ‘Coke Studio Africa’.

Habari kutoka katika chanzo cha kuaminika jijini Nairobi zinaeleza kuwa Ali Kiba amepangiwa kutengeneza wimbo na kuperform na mmoja kati ya mastaa wa kike mwenye jina nchini Kenya na Nigeria.

Wawili hao watashirikiana kufanya wimbo utakaotayarishwa na Owuor Arunga ambaye ni mshindi wa tuzo za Grammy na mkali wa kupiga trumpet. Anajulikana zaidi kwa kazi alizoshirikiana na rapa wa Marekani, Maclemore.
DSC_0545
Ali Kiba ambaye ni mshindi wa tuzo sita za KTMA ameachia video mpya ya wimbo wake ‘Chekecha Cheketua’ ambayo imeanza kufanya vizuri katika kituo cha Trace Africa.

Chile Yaitendea Haki Ardhi Ya Nyumbani, Yazisubiri Argentina Na Paraguay
Kocha Mkongwe Akubalia Kuachia Ngazi Uholanzi