Miezi sita baada ya kufanikiwa kutoroka kwenye gereza lenye ulinzi mkali nchini Mexico, bilionea maarufu wa dawa za kulevya,  Joaquin “El Chapo” Guzman amekamatwa na jeshi la nchi hiyo.

Taarifa za kukamatwa kwa El Chapo zimetolewa kwa mara ya kwanza na rais wa nchi hiyo, Enrique Peña Nieto kupitia akaunti yake ya Twitter.

“Mission accomplished: We have him. I want to inform the Mexicans that Joaquin Guzman Loera has been detained” alitweet rais wa Mexico.

El Chapo3

Tajiri huyo wa unga mwenye utajiri unaokariwa kuwa zaidi ya $1 billion alitoroka kwenye gereza lenye ulinzi mkali zaidi nchini humo akipitia kwenye mfereji wa maji machafu unaotokea ndani ya bahari. Ilikuwa ni mara ya pili kwa tajiri huyo kutoroka gerezani baada ya kukamatwa na kukaa jela wiki 16 pekee.

El Chapo4

Wakati huu, El Chapo alikamatwa akiwa na msaidizi wake wa karibu zaidi. Katika zoezi la kumkamata, walinzi wake watano waliuawa na wengine sita wakamatwa na Polisi wakati wa kurushiana risasi katika mji wa Los Mochis.

Yaya Toure: Mimi kuikosa Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika ni Aibu Kwa Afrika
Lissu awatofautisha Tuhuma za Ufisadi za Lowassa na Profesa Muhongo