Imedhihiri rasmi uwanja wa FC Barcelona ‘Camp Nou’ kuuvunja ili kupisha ujenzi mpya wa Uwanja huo ambao ulikuwa unachukuwa mashabiki 99, 354 walioketi.

Picha kadhaa zimesambaa katika Mitandao ya Kijamii zikionesha sehemu za Uwanja huo zikivunjwa na vifaa maalum, kuanzia jana Jumatatu (Julai 10).

Taarifa zinaeleza kuwa ujenzi mpya wa Uwanja wa Camp Nou unatarajiwa kutumia kiasi cha Pauni Bilioni 1.25, na utakuwa tayari kabla ya kuanza kwa msimu wa 2025/26.

Matengenezo hayo yatauwezesha Uwanja wa Camp Nou kuchukuwa mashabiki 105,000, na utakuwa Uwanja mkubwa zaidi Barani Ulaya, ukifuatiwa na Wembley uliopo England wenye uwezo wa kuchukuwa Mashabiki 90,000 walioketi.

Muonekano wa Uwanja wa Camp Nou utakavyokuwa baada ya ujenzi mpya

Uwanja wa Camp Nou pia unatarajiwa kuwa na Paa kubwa ambalo litanakshiwa na rangi za Klabu ya Barcelona, ambapo sehemu hiyo inatarajiwa kugharimu Pauni Milioni 237.

Muonekano wa Paa la Uwanja wa Camp Nou baada ya kukamilika kwa ujenzi mpya

Zaidi ya wafanya kazi 250 wanatarajiwa kuwa kazini kwa kipindi cha miaka miwili, ili kufanikiwa ujenzi wa Uwanja huo, ambao utaanza mara moja baada ya zoezi la kubomia kukamilika.

Huo unakuwa ni ujenzi wa kwanza mkubwa katika Uwanja huo tangu ule wa kwanza kufanywa mwaka 1957.

Mchezo wa mwisho kuchezwa Uwanjani hapo ulikuwa kati ya wenyeji dhidi ya Real Mallorca ambao ulimalizika kwa FC Barcelona kushinda 3-0.

Mpango wa ujenzi wa Uwanja wa Camp Nou, ulitangazwa hadharani na Uongozi wa FC Barcelona Julai 2022, na michezo ya Klabu hiyo kwa msimu ujao 2023/24, itachezwa katika Uwanja wa Olympic.

Moses Phiri afunguka usajili Simba SC
Kyle Walker ajiweka njia panda Man City