Boss wa WCB, Diamond Platinumz amewapeleka wasanii na viongozi wa lebo hiyo kwa Rais mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete ikiwa ni hatua ya kuitambulisha rasmi lebo hiyo kwake na kumjulia hali.

Wasanii hao pamoja na viongozi wameonekana katika picha mbalimbali wakifanya mazungumzo na mkuu huyo wa Serikali ya Awamu ya Nne pamoja na mkewe, Mama Salma Kikwete.

“Earlier today at our Tanzanian former President @JMKikwete House… (Mapema leo tukideka kwa Mzee wetu Mh Rais Mstaaf @JMKikwete ….),” ameandika Diamond kwenye picha aliyopost Instagram inayowaonesha wakiwa na Dk. Kikwete.

diamond-na-kikwete

Dk. Kikwete ni mmoja kati ya marais waliokuwa marafiki wakubwa wa wasanii nchini. Wakati akiwaaga wasanii kama Rais wa Serikali ya awamu ya nne, aliahidi kuendelea kushirikiana nao akiwa kama ‘mwananchi maarufu’.

kikwete-mama-salma-na-wcb

Mwanafunzi Kidato cha Kwanza ajifungua bwenini
Gavana BOT afichua siri ya kilio cha fedha kupotea mtaani