Hatimaye, Diamond Platinumz na mpenzi wake Zari wa Uganda wamemkaribisha duniani mtoto wao wa kike waliyembatiza jina la Tiffah.

Zari alijifungua salama jana majira ya saa kumi usiku ambapo kwa mapenzi ya mwanae wa pekee, Diamond alikuwepo hospitali akisubiri kuanzia majira ya saa saba usiku.

Kupitia Instragram, Diamond amepost picha inayomuonesha mama yake mzazi akimbeba mjukuu wake na kuandika ujumbe kuonesha furaha yake toka moyoni.

“My mom’s face it’s enough to Express how i feell… Welcome to the world @princess_tiffah. Sura ya mama yangu inatosha kueleza ni kiasi gani najiskia ndani ya Moyo wangu… karibu kwenye ulimwengu @princess_tiffah,” aliandika.

Mbatia Asema Yake Baada Ya Profesa Lipumba Kung’atuka Uenyekiti CUF
Kim Kardashian, Kanye West ‘Waselfika’ Na Hillary Clinton