Mwaka jana (2015) mtandao mmoja wa Afrika, uliwataja ‘Ma-First Lady’ 10 wa Afrika ambao wanaaminika kuwa ni warembo zaidi kuliko wengine. Orodha hiyo ilitolewa na kuchambuliwa na timu ya wahariri wa mtandao huo huku ikiwaachia wasomaji kutoa maoni yao.
10: Margaret Gakuo Kenyatta (Kenya)
Huyu ni mke wa Rais Uhuru Kenyatta ambaye ana umri wa miaka kati ya 50 na 51. Licha ya kuwa na umri huo, sura yake na muonekano wake ‘simple’ unamfanya awe na mvuto wa aina yake huku nywele nyeupe zikimpa utambulisho wa aina yake.
Baadhi husema anaonekana ana aibu pale anapokuwa mbele ya hadhara, lakini hilo linamuongeza uzuri wake.
 9: Dominique Folloroux-Ouattara (Ivory Coast)



Alikuwa mwanamitindo maarufu nchini humo na mhudumu wa ndege (air hostess). Kazi iliyompelekea kukutana na mpenzi wake ambaye sasa ni rais wa Angola, Jose Eduardo Dos Santo.

5: Zeinab Suma Jammel (Gambia)

4: Hinda Deby Itno (Chad)
Hinda Deby, ni mwanamke mrembo anayependa mitindo ya mavazi na mpole. Muda mwingi amekuwa akivaa magauni mazuri yanayo-oana rangi na mitandio yake.
Pamoja na kuufunika mwili wake kwa mitandio na magauni marefu, bado uzuri wake huonekana dhahiri.
3: Chantal Biya (Cameroon)
Chantal Biya ni ‘first lady’ Â mrembo haswa, anayependa mitindo ya mavazi na kujiweka sawa kichwani kwa mitindo mbalimbali ya nywele. Mavazi mengi anayopendelea kuvaa huwa katika mtindo unaoendana na utamaduni wa nchi yake.
2: Princess Lalla Salma (Morocco)
Princess Lalla Salma ni mke wa Mfalme wa Morocco, Mohammed VI. Huyu ni mwanamke mzuri sio tu kwa sura lakini hata kiakili yuko ‘smart’ sana.
Kutokana na shughuli mbalimbali anazozifanya, amekuwa na ushawishi mkubwa kwa serikali ya Morocco.
1: Sylvia Bongo Ondimba (Gabon)
Sylvia Bongo ametajwa kuifunika orodha hii ya wake za Marais wa Afrika wanaotajwa kuwa warembo zaidi. Sylvia pia anapewa nafasi ya kuingi kwenye orodha ya wake wa Marais warembo zaidi duniani.
Wapo ma-first lady wengi waliojaliwa uzuri na urembo, lakini mtazamo umewapa nafasi 10 za juu zaidi hawa.
Je, unaionaje hii orodha na ni yapi maoni yako?