Kikosi cha Young Africans kimeweka kambi kwenye majengo maarufu ya Avic yaliyojitenga na yenye utulivu mkubwa na vifaa kibao vya michezo ukiwemo uwanja wa ndani kwa ndani na hakuna mgeni anayeruhusiwa kuingia ndani bila ruhusa maalumu.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya klabu hiyo, Uongozi kwa kushirikiana na wadhamini kampuni ya GSM umeamua kikosi chao kitakuwa kinaishi hapo kuanzia sasa na hakuna habari ya hotelini tena kwani hapo ni pazuri zaidi na kocha amepakubali.

Ukifika eneo hilo unakutana na ukuta mrefu na ndani yake tena kuna ukuta mwingine uliopishana kama nusu kilomita na ndani ya ukuta wa pili ndio kuna majengo mbalimbali ya makazi mapya ya Young Africans.

Navalny alifanyiwa jaribio la mauaji - Merkel
Majaliwa avunja makundi CCM

Comments

comments