Mwimbaji Jennifer Lopez alipata ajali ya aina yake alipokuwa katika show yake ya ‘All I Have’ iliyofanyika Las Vegas nchini Marekani na kupelekea moja kati ya sehemu zake za siri kuonekana.

J Lo mwenye umri wa miaka 46 alipata ajali hiyo wakati alipokuwa akijaribu kuwashukuru mashabiki kwa muitikio wao ikiwa ni dakika chache amalize show.

Aliinama (bow) pamoja na wachezaji wake aliowashika mikono, ndipo nguo yake laini iliposhindwa kuhimili na kuachia sehemu za makalio na kuonesha kile ambacho hakipaswi kuonekana katika eneo kama hilo.

Shabiki mmoja aliyekuwa anafuatilia onesho hilo alifanikiwa kuchukua picha ya tukio hilo na baadae mtandao wa TMZ uliweka video.

Mbunge atimuliwa kwenye kikao na Polisi
Diamond autaka uwaziri wa Nape