Timu ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, leo imeanza mazoezi ikiwa nchini Kenya ilipokwenda kushiriki michuano ya kombe la Challenge itakayoanza kutimua vumbi lake jumapili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kutoka mjini Nairobi kupitia kitengo cha habari cha shirikisho la soka nchini TFF, wachezaji wote wapo katika hali nzuri na leo walifanya mazoezi kwenye uwanja wa Machakos Academy.

Mazoezi ya timu hiyo yamefanyika asubuhi na jioni.

Kilimanjaro Stars imepangwa katika kundi A la michuano hiyo, na itaanza kucheza dhidi ya Libya siku ya jumapili.

  Timu ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, ikijifua leo kwenye Uwanja wa Machakos Academy.

Wema aibwaga Chadema, arudi CCM
Makundi ya fainali za kombe la dunia 2018 hadharani