Kokosi cha timu ya taifa ya Tanzania bara (Kilimanjaro Stars) kimeanza maandalizi ya kujiwinda na michuano ya kombe la Challenge itakayoanza mwishoni mwa juma hili nchini Kenya.

Kilimanjaro Stars inayonolewa na kocha Ammy Ninje, inafanya mazoezi kwenye uwanja wa Gymkhana jijini Dar es salaam huku wachezaji karibu wote walioitwa kikosini wakiripoti.

Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A sambamba na Zanzibar, Rwanda, Libya na wenyeji Kenya. Itaanza kampeni ya kuwani ubingwa wa Challenge 2018 kwa kucheza dhidi ya Libya Novemba 03 mjini Nakuru.

Timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, wakifanya mazoezi mbalimbali katika Uwanja wa Gymkhana, Dar es Salaam leo Novemba 28, 2017. Kilimanjaro Stars inajiandaa kucheza Kombe la Chalenji 2017 huko Kenya kuanzia Desemba 3, mwaka huu.

Samia Suluhu amtembelea Lissu jijini Nairobi
Majaliwa atoa onyo kwa watumishi