Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Dk. John Magufuli ametangaza vita dhidi ya wakuu wa mikoa ambao wananchi wao watasikika wakilia kuwa wamekumbwa na baa la njaa.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa kwenye ziara yake jijini Arusha ikiwa ni sehemu ya safari yake kuelekea Wilayani Monduli anapokwenda kuhitimisha mafunzo ya kijeshi ya kuonesha uwezo wa medani mwaka huu, yanayofanyika katika Briged ya 303.

Pia, anatarajiwa kutoa kamisheni kwa askari wanafunzi katika chuo cha mafunzo ya kijeshi cha TMA Monduli.

Magufuli, gwanda 2

Amesema kuwa hataki kusikia tena kilio cha wananchi kuhusu suala la njaa na kusisitiza kuwa Mkuu wa Mkoa ambaye wananchi wake watalia kuwa na njaa atawaadhibu ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi.

Rais aliwahakikishia wananchi kuwa ataendelea kupambana na rushwa bila kukoma hadi atakapoiondoa kero hiyo kwa wananchi.

1 Magufuli 3

 

Wamiliki wa IPTL wamburuza Zitto mahakamani, wadai alikuwa na 'Maslahi' kwenye Tegeta Escrow
Haruna Niyonzima Arejea Kundini