Mara baada ya kuibuka na ushindi wa magoli matatu kwa sifuri dhidi ya Kagera Sugar, kikosi cha KMC FC leo kimeanza maandalizi ya kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ sambamba na michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania pamoja na Coast Union ya Tanga.

KMC itacheza mchezo wa ‘ASFC’  Ijumaa (Februali 26) dhidi Kurugenzi ya Mkoani Simiyu utakaopigwa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine vijana wa Kino Boys wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri na hivyo kuibuka na ushindi katika michezo huo.

Baada ya mchezo huo wa ‘ASFC’ KMC FC itakuwa ugenini katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo itaanza na Polisi Tanzania Machi 04 katika uwanja wa Sheikh Amri  Abeid jijini Arusha, na kisha mchezo utakaofuata utawakutanisha dhidi ya Coast Union Machi 07 katika uwanja wa Mkwawani jijini Tanga.

“Tumemaliza mechi yetu ya Ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar, na sasa tunajipanga katika mchezo wa kombe la ASFC, tunajua mchezo utakuwa mgumu kutokana na kwamba wapinzani wetu ndio tunakutana nao kwa mara ya kwanza, hivyo tunajipanga ilituweze kupata matokeo katika mchezo huo.

“Tulifaya vizuri katika michezo yetu miwili ambayo tulikuwa nyumbani, sasa tunakwenda kucheza michezo yetu mwili tukiwa ugenini, ligi ni ngumu na tunafahamu kuwa kila Timu inahitaji matokeo, lakini kama KMC FC tunapambana kuhakikisha kwamba tunafanya vizuri katika michezo yetu hiyo miwili.”

Hadi sasa KMC FC ipo katika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi kuu Tanznaia Bara ikiwa imecheza michezo 21 na kufikia alama 31, hivyo mkakati ni kuhakikisha inafanya vizuri katika michezo inayofuata na hivyo kuendelea kupanda katika nafasi za juu.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Februari 23, 2021
PICHA: Maandalizi dhidi ya Al Ahly yakamilika