Mgombea urais anayewakilisha kambi ya Ukawa ameendelea na harakati zake za kukutana na wananchi wa kipato cha chini ambapo leo amefanya ziara ya kushitukiza katika soko la Tandale, jijini Dar es Salaam.

Lowassa ameingia katika soko la Tandale mapema leo asubuhi akiwa na mgombea mwenza, Juma Haji Duni ambapo amepokelewa kwa shangwe na wafanyabiashara ndogondogo katika soko hilo. Mbali na kuzungumza naokwa nia ya kufahamu matatizo yanayowakuta, Lowassa ameshiriki nao kupata kinywaji kwa kutumia kikombe alichopewa na mmoja ya wafanyabiashara hao.

L2

Jana, Edward Lowassa na Juma Haji Duni waliwatembelea wananchi wa maeneo ya Gongo la Mboto kwa kushitukiza na kisha kupanda usafiri wa daladala huku wakizungumza na abiria na wafanyakazi wa daladala kufahamu matatizo yanayowakuta.

L3

 

L4

L 5

Duru zimeeleza kuwa mgombea huyo amepaga kuzunguka katika maeneo ya Dar es Salaam kwa kushitukiza kwa muda wa wiki nzima kabla ya kufanya uzinduzi rasmi wa kampeni, Agosti 29 mwaka huu katika viwanja vya Jangwani.

Joh Makini Akamilisha Video Na Rapa AKA Wa Afrika Kusini
Mwadui FC Kujipima Kwa Mabingwa Wa Kagame CUP