Kocha Mkuu wa Azam FC mpya, George Lwandamina, amewasili jijini Mwanza tayari kwa kuanza kazi ya kukinoa kikosi cha klabu hiyo, ambacho kitakabiliwa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Gwambina FC, Jumatatu (Desemba 07).

Lwandamina amewasili jijini humo akiwa sambamba na Afisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’ na Makamu Mwenyekiti, Omary Kuwe.

Kocha Lwandamina aliyesaini mkataba wa miaka miwiwli jana Alhamis jijini Dar es salaam, anatarajiwa kuwa sehemu ya benchi la ufundi wakati kikosi chake kitakapokua kikisaka alama tatu muhimu dhidi ya Gwambina FC.

Azam FC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kucheza michezo 13, iliyowapa alama 26, huku ikifunga mabao 19.

New Habari 2006 yasitisha uzalishaji wa magazeti yake
Gareth Bale afikisha la 200

Comments

comments