Mabingwa wa soka barani Ulaya (timu ya taifa ya Ureno) wamepokelewa kishujaa walipofika mjini Lisbon wakitokea Ufaransa zilipofanyika fainali za Euro 2016.

Mashabiki pamoja na viongozi wa serikali walijitokeza kuwalaki wachezaji pamoja na maafisa wengine wa soka nchini humo, walioandamana na timu ya Ureno ilipokua nchini Ufaransa ambapo usiku wa kuamkia jana ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa barani Ulaya kufuatia ushindi wa bao moja kwa sifuri.

Ndege iliyokuwa imewabeba, wachezaji pamoja na maafisa wa soka nchini Ureno, ilipowasili katika uwanja wa ndege wa mjini Lisbon, ilimwagiwa maji yenye rangi nyekundu na kijani, ikiwa ni kiashirio cha bendera ya taifa hilo.

Baada ya kushuka kwenye ndege wachezaji walipanda katika basi la wazi lililokua limeandaliwa, na kupita katika mitaa mbali mbali ya mjini Lisbon ambayo ilikua imesheheni mashabiki.

Ureno wametwaa kombe la Euro 2016 hilo kwa kuifunga Ufaransa ambao ni wenye kwa bao 1-0.

Kabla ya kufika katika hatua ya fainali Ureno walipitia changamoto kadhaa za kupambana, na ifuatayo ni ratiba iliyowakabili.

Hatua Ya Makundi: Ureno 1-1 Iceland

Hatua Ya Makundi: Ureno 0-0 Austria

Hatua Ya Makundi: Hungary 3-3 Ureno

Hatua Ya 16 Bora: Croatia 0-1 Ureno (Muda Wa Nyongeza-AET)

Hatua Ya Robo Fainali: Poland 1-1 Ureno (Ureno Walishinda Kwa Penati 3-5)

Hatua Ya Nusu Fainali: Ureno 2-0 Wales

Hatua Ya Fainali: Ureno 1-0 France (Muda Wa Nyongeza-AET)

Daraja la Nyerere lakusanya Bilioni za wenye magari, pikipiki, bajaji
Video: Waziri Mahiga amepokea msaada wa maadawati