Madaktari wamefanikiwa kufanya upasuaji na kuwatenganisha watoto mapacha wakiwa na siku nane tu baada ya kuzaliwa wakiwa wameungana.

Jopo la Madaktari 13 lililoundwa jijini Bern nchini Uswizi walifanya upasuaji huo uliokuwa hatari zaidi na kuwatenganisha mapacha hao wa kike, Lydia na Maya ndani ya saa tano ndani ya chumba cha upasuaji.

Watoto hao walikuwa wameungana kwenye ini, lakini walikuwa na viungo vyote muhimu. Madaktari walieleza kuwa upasuaji huo ulifanywa huku kukiwa na asilimia 1 pekee ya kufanikiwa.

watoto 2

Vyombo vya habari nchini hum0o vilieleza kuwa mapacha hao waliofanyiwa upasuaji Disemba 10 mwaka jana, wanaendelea vizuri na wameanza kunyweshwa maziwa na chakula.

watoto 3

Kikwete apata uteuzi mwingine mzito wa kimataifa
Meli Kubwa yazua taharuki, Yabembelezwa isizame